KANISA KATOLIKI YAKANA RIPOTI YA AU KUHUSU UDHALILISHAJI WA MAPADRI NA MAASKOFU DHIDI YA WATOTO

Posted in
No comments
Thursday, February 6, 2014 By danielmjema.blogspot.com

Uongozi wa kanisa katoliki duniani mjini Vatican umelaani vikali ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa hapo jana ikilituhumu kanisa hilo kuwalinda mapadri na maaskofu ambao wanatuhumiwa kuhusika na vitendo vya udhalilishaji dhidi ya watoto.


POPE FRANCIS

 

Mara baada ya kutolewa kwa ripoti ya UN inayokemea sera za kanisa hilo pamoja na viongozi hao wa kidini kulindwa na uongozi wa juu wa kamati ya Papa, bado kanisa hilo limedai ripoti hiyo ni ya uongo na inayopandikiza chuki kwa waumini wake kwa kuwa kwa sehemu kubwa imetekeleza mapendekezo mengi ambayo yametolewa na tume ya Umoja wa mataifa iliyokuwa ikichunguza tuhuma za udhalilishaji wa watoto dhidi ya kanisa hilo.

Wakati wamahojiano yao na kamati maalumu ya Umoja wa Mataifa majuma kadhaa yaliyopita, viongozi wa kanisa hilo walikiri kuwepo kwa vitendo hivyo na kwamba kesi nyingi wamezishughulikia kama kanisa na ni masuala yanayohusu imani zaidi.

Ripoti ya UN inalitaka kanisa hilo kuwakabidhi mapadri na maaskofu waliohusika na vitendo hivyo kwa vyombo vya usalama, pamoja na kuondoa ukiritimba wa upatikanaji wa taarifa muhimu za ndani ya kanisa hilo kuhusu matukio kama haya.
 
CHANZO:RFI/SWAHILI

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .