WANAWAKE WALIOBAKWA KUFUATIA MAPIGANO LIBYA KUFIDIWA
No comments
Thursday, February 20, 2014
By
danielmjema.blogspot.com
![]() |
| Wanawake wa Libya waliathiriwa zaidi na vita nchini humo |
Waziri wa Sheria nchini Libya
,salaha al-Marghani,amesema kuwa Baraza la mawaziri limekubaliana kuwa
Wanawake waliobakwa wakati wa harakati na maandamano ya kuuangusha
utawala wa aliyekuwa Rais wa taifa hilo Muammar El Gaddafi mwaka 2011
watambuliwe kuwa waathirika wa vita.
Mahakama ya kimataifa ya uhalifu imekusanya ushahidi kuwa vikosi vya waliokuwa wakimuunga mkono Gaddafi walitekeleza vitendo vya ubakaji kama silaha.
Inaelezwa kuwa Wanawake wanaobakwa mara nyingi wamekuwa wakitengwa nchini Libya, hivyo haijafahamika wanawake wangapi watajitokeza.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako


0 MAOINI :