MTANZANIA Jackline
Sakilu amewatuliza Watanzania kwa kuibuka mshindi katika mbio za mwaka huu za
Kimataifa za Kilimanjaro Marathon.
|
Mshindi wa
kwanza wa Half Marathoni ,Jackline Sakilu akihitimisha mbio. |
Sakilu ambaye
anatokea katika Jeshi la wananchi la Tanzania (JWTZ), amefanya hivyo jana
katika mbio za Kilomita 21 wanawake, akikimbia kwa muda wa saa 1:12:43 mbele ya
wanariadha kutoka nchi jirani ya Kenya.
Katika nafasi
ya pili alikuwa ni mwanariadha Cynthia Towett, aliyekimbia kwa muda wa saa
1:14:33, na katika nafasi ya tatu alikuwa ni Naomi Maiyo aliyekimbia kwa muda
wa saa 1:17:47 wote kutoka Kenya.
Katika mbio hizo
kwa upande wa wanaume, nafasi ya kwanza alikuwa ni Alfred Lagat kutoka Kenya
ambaye alikimbia kwa muda wa saa 1:02:34 akifuatiwa na Wakenya wenzake Silah
Limo (1:03:04) na Keneth Kandie (1:03:20) huku Mtanzania wa pekee katika kumi
bora, Alfred Felix, kutoka Klabu ya riadha ya Holili (HYAC) akishika nafasi ya
tano (1:03:27).
Wakati huo huo
zimwi la kufanya vibaya katika mbio ndefu (Kilomita 42) imeendelea kuiandama
Tanzania baada ya Wanariadha kutoka Kenya kutawala mbio hizo kwa mwaka mwengine
tena.
Katika Mbio za
wanaume, Mshindi wa kwanza David Ruto kutoka Kenya aliyetimua
mbio hizo kwa muda wa masaa 2:16:04,nafasi ya pili alikuwa ni Julius Kilimo (2:16:17)
na nafasi ya tatu ikishikwa na Victor Serem 2:16:32 huku Mtanzania wa kwanza
katika mbio hiozo kwa upende wa wanaume, Daudi Lwabe, akiingia katika nafasi ya
nane akitumia muda wa masaa 2:18:34.
Katika upande
wa wanawake mshindi alikuwa ni Frida Lodera aliyetumia muda wa masaa 2:40:11, nafasi
ya pili ni Joan Rotich aliyetumia muda wa masaa 2:42:46 na nafasi ya tatu
ikashikwa na Abigal Toroitich ambaye alitumia muda wa masaa 2:55:14 ambapo
Mtanzania pekee aliyeingia kumi bora, Banuelia Bryton, akiingia katika nafasi ya tisa kwa kutumia
muda wa masaa 3:12:26.
|
0 MAOINI :