DIAMOND AWA BALOZI WA "MZIIKI"

No comments
Thursday, September 25, 2014 By danielmjema.blogspot.com


Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya, Naseeb Abdul a.k.a Diamond Platinumz akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutangaza ushirikiano wake na kampuni inayoendesha programu ya Mziiki.Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Spice VAS Africa wanaoendesha programu hiyo ya Mziiki,Arun Nagar na kushoto ni Meneja wa Diamond Platinumz,Babu Talle.

Mkali wa Bongo Flava Tanzania Diamond Platnumz amepewa nafasi ya kushirikiana na Mziiki kama Brand Partner. Msanii huyu ambaye amefanikiwa kushinda tuzo mbalimbali amekuwa wa kwanza kutia saini kama Brand Partner na tayari ni mmoja wa mamia ya wasanii pekee wa Afrika walio katika program ya muziki unaopendwa zaidi Afrika kupitia simu za kiganjani pamoja na kuwa mwakilishi wa bidhaa hiyo akiwakilisha nchi yake.

"Tunafurahi kwamba Diamond Platnumz kwa sasa ni Brand Partner wa Mziiki," anasema Arun Nagar, Mkurugenzi Mtendaji wa Spice VAS Africa, watengenezaji wa Mziiki. "Kwa kushirikiana na msanii mwenye kiwango kama Diamond pamoja na mashabiki wake ni hatua nzuri kwa Mziiki.

Ushirikiano kama huu unaonyesha dhamira yetu ili kuendelea kuhakikisha kwamba watumiaji wetu na muziki bora wa Afrika unawafikia pale walipo na tutaweza kufanya kazi karibu na Diamond na kupanua wigo wa wateja wetu na kuwapatia mashabiki wake zaidi ya kile walichotarajia. Nadhani pia ni ushahidi wa ukweli kwamba sisi tumechukua nafasi kubwa katika ulimwengu wa muziki streaming na wapenzi wa muziki wa Afrika wanapaswa kukumbuka hilo. "

Mziiki ni huduma pekee inayokupa Miziki ya kiafrika kupitia Streaming, huduma ambayo inatoa safu mbalimbali ya muziki kutoka Afrika na kimataifa. "Mimi nimepata mzuka kujiunga na Mziiki," anasema Diamond. "Programu na simu (mobi) tovuti ni nafasi kubwa kwa ajili ya wasanii kupanua idadi yao ya mashabiki na kutambulisha mara ya kwanza single yao mpya kusikika bara la Afrika na dunia."

Mziiki ni programu ya simu iliyoundwa kwa ajili ya Music Streaming iliyosheheni miziki ya Afrika. Imepata umaarufu haraka ikiwa na mkusanyiko mkubwa wa sauti safi na vipaji kipekee vinavyokidhi miziki ya kiafrika.Programu hii ni rahisi kutumia,ina makala ambayo huruhusu mtumiaji kushirikisha marafiki wimbo waupendao au kuwatumia nyimbo kama miito ya simu ya nyimbo walizochagua. Makala haya yamewekwa kuwawezesha wasanii, kama Diamond, kufikia mashabiki wapya katika Afrika na duniani kote.

"Mziiki kweli imenipa zaidi ya kile ambacho ningeweza kuomba" Anasema Diamond. "Mimi si tu kuwapatia mashabiki wangu nafasi ya kupata nyimbo zangu zote bali pia pia kupata nafasi ya kupanua wigo wa mashabiki wangu kupitia programu ya “Share and Dedicate” . Wakati mashabiki wangu wakishirikisha au wakituma wimbo wangu wowote maalum kwa wenzao,nani ajuaye waweza kusambaa kwa kiasi gani? Mimi tayari nimeshaanza kuona idadi ya mashabiki wangu ikiongezeka kwa namna hii.

Ikiwa na kiwango kizuri na kuongezeka kwa orodha ya wasanii waliosajiliwa kutoka katika bara la Afrika, Mziiki ni mahali ambapo wasanii wapya wanaweza kwenda kuzindua kazi zao na wasanii waliopo sasa kuendelea kukua.

Mziiki ni program ya Mobile Streaming iliyoundwa ili kukidhi mahitaji ya msanii na mashabiki kwa jumla. Mziiki ilianzishwa mwezi Mei 2014, na imesaidia kuongeza mafanikio katika kazi za wasanii na inaendelea kukua kila siku na kuwawezesha wasanii kufurahia zaidi kama ilivyo kwa Diamond Platnumz..

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .