CRDB YAKABIDHI VIFAA VYA MICHEZO KWA VIONGOZI WA DINI

No comments
Monday, October 6, 2014 By danielmjema.blogspot.com


Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei (wa tatu kushoto) akimkabidhi sehemu ya vifaa vya michezo Mwenyekiti wa Kamati ya Amani ya Viongozi wa Dini, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhad Mussa Salum kwa ajili ya mechi ya viongozi wa Kamati ya Amani na Ushirikiano inayowaunganisha viongozi wa dini zote itakayofanyika Oktoba 12 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa, Katibu wa Kamati hiyo, Padri John Solomon (wa pili kulia),  Mkurugenzi wa Tawi la Benki ya Kijitonyama, Lucas Busigazi (kushoto) na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mchungaji George Fupe (wa pili kushoto). 

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles kimei akizungumza na waandishi wa habari.
Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum akionyesha jezi namba 9 atakayoitumia katika mchezo huo.
Dk. Kimei akifurahia jambo wakati wa makabidhiano ya vifaa vya michezo kwa viongozi wa timu ya Kamati ya Amani na ushirikiano ikiwa ni maandalizi ya mechi baina ya viongozi wa madhehebu ya dini.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .