MWANASHERIA MKUU WA ZANZIBAR AKAMATWA BAADA YA KUPIGA KURA YA "HAPANA".
Posted in
Matukio
No comments
Wednesday, October 1, 2014
By
danielmjema.blogspot.com
Taarifa ambazo hazijathibitishwa zinasema kuwa, leo muda mfupi uliopita Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Othman Masoud baada ya kupiga kura ya wazi ya Hapana kuhusu katiba amekamatwa na watu wa idara ya usalama na sasa yupo njiani akirejeshwa Zanzibar kama ni kweli anapeleka Zanzibar ama Mambwepande .......
Hali hii ni ya hatari na Dodoma tayari kuna tayahari kubwa sana ,ila hali inawez kuchafuka wakati Wowote visiwani Zanzibar kutokana na uonevu huu ambao unafanywa na watawala wa CCM .
Hali ilikuwa mbaya Sana mara baada ya kupiga kura kwani wabunge wa CCM znz walitaka kumpiga ndio akalazikima kutolewa ukumbini chini ya ulinzi mkali na kufungiwa kwenye ofisi moja akiwa ameandamana na Pandu Ameir Kificho, Balozi Seif Idd, Nahodha, Pinda na baada ya muda aliondolewa hapo Akiwa ameandamana nafPandu Kificho kwenye gari yake kupitia lango la Waziri Mkuu akiwa ameambatana na msafara wa maafisa usalama, na kupelekwa Airport
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :