KAMANDA WA UJERUMANI AJIVUNIA USALAMA BAHARI YA HINDI

Posted in
No comments
Monday, December 8, 2014 By danielmjema.blogspot.com

DSC_0001

Balozi wa Ujerumani nchini Mh. Egon Kochanke (kushoto) akizungumza na wageni waalikwa wakiwamo viongozi mbalimbali wa Serikali na mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao Tanzania kwenye hafla maalum ya kuwakaribisha na kuwapongeza wanajeshi wa kikosi cha wanamaji wa meli ya kivita ya Ujerumani FGS Lübeck, inayofanya doria katika ukanda wa Bahari ya Hindi kama sehemu ya jeshi la kimataifa linaloendesha operesheni Atalanta chini ya kamanda Peter Christian Semrau (kulia) iliyofanyika ndani ya meli hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa juma.(Picha zote na Zainul Mzige wa MOblog).

Na Mwandishi wetu
KAMANDA wa meli ya kivita ya Ujerumani FGS Lübeck, inayofanya doria katika ukanda wa Bahari ya Hindi kama sehemu ya jeshi la kimataifa linaloendesha operesheni Atalanta, Peter Christian Semrau, amesema jumuiya ya kimataifa imepata mafanikio makubwa kwa kuwezesha njia inayotumika sana na meli kuwa salama.

Akizungumza katika mahojiano ndani ya meli hiyo ambayo imetia nanga katika bandari ya Dar es Salaam, Kamanda Semrau alisema kwamba kwa mwaka huu hapakuwepo na tukio kubwa ambalo limetikisa eneo hilo la Pwani ya Pembe ya Afrika inayopakana na Somalia na Yemen.

Alisema kuanzia shughuli za kimataifa kukabili uharamia na ujambazi baharini kuanza mwaka 2009 kumekuwepo na ushindi wa kimataifa kutokana na kuendelea kupungua kwa matukio katika eneo hilo ambapo awali ilikuwa ni tishio kubwa.

Alisema pamoja na kupungua kwa matukio ya kijambazi na utekaji nyara kazi ambayo inatarajiwa kufanywa mwakani ni kuhakikisha kwamba mataifa yanayopakana na bahari ya Hindi yanawezeshwa kujilinda yenyewe dhidi ya matukio ya baharini.

DSC_0004
Pichani juu na chini baadhi ya viongozi wa serikali ya Tanzania na mabalozi mbalimbali waliojumuika kwenye hafla hiyo wakisiliza risala ya Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Mh. Egon Kochanke (hayupo pichani).

Meli hiyo ambayo inafanya doria kuanzia kaskazini mwa Afrika hadi Kusini imetia nanga Dar es salaam ikitokea Madagascar ambako nako ilipata mapokezi makubwa. Operesheni Atalanta inaendeshwa na vikosi vya Umoja wa Ulaya vikilinda eneo la bahari ambalo lina shughuli nzito kwa meli za biashara Meli hiyo ambayo itakuwa katika operesheni hadi februari mwakani itapokewa kazi hiyo na meli nyingine ya FGS Bayern.

Naye Balozi wa Ujerumani nchini Mh. Egon Kochanke akizungumza na waandishi wa habari akiwakaribisha katika melivita hiyo alisema kwamba amefurahishwa na mchango wa taifa lake katika kuhakikisha pwani ya Bahari ya Hindi upande wa Afrika inakua salama na watu wanapata huduma zinazotakiwa.

DSC_0005
Alisema moja ya kazi kubwa ya meli hiyo ni kusindikiza meli zenye vyakula au huduma mbalimbali za kijamii kwa mataifa ambayo yanashida ili kupunguza maumivu. Alisema pamoja na meli hiyo kutia nanga Dar es Salaam kuonesha ushirikiano wa kutosha kati ya taifa lake na Tanzania, anatarajia mwakani mahusiano ya Tanzania na Ujerumani yatazidi kuimarika hasa katika nyanza za hifadhi na maendeleo ya jamii.

Aidha balozi huyo alisema kwamba taifa lake linaongeza fedha zaidi kwa ajili ya uanzishaji wa mamlaka ya wanyamapori nchini Tanzania kwa lengo la kuifanya iwe na nguvu na uwezo wa kulinda wanyama hao.

Pia alisema inafikiria namna ya kufanya na meli ya MV Liemba ambayo alisema ni moja ya vielelezo hai vilivyopo vyenye maana kubwa katika uhusiano wa Tanzania na Ujerumani.
DSC_0006
Alisema meli hiyo inafaa kufanyiwa ukarabati ili kuweza kutoa huduma kandoni mwa ziwa Tanganyika. Aidha alisifu ukuaji wa demokrasia nchini Tanzania hasa kwa kuzingatia uhuru uliopo wa vyombo vya habari na majadiliano yenye afya bungeni yenye lengo la kujenga taifa lenye nguvu.

Aidha alisema Ujerumani itaendelea kukuza uhusiano na Tanzania ambayo ni nanga ya usalama kwa mataifa ya Afrika Mashariki na ukanda wa Bahari ya Hindi kwa upande wa Afrika.

DSC_0015
Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Mh. Egon Kochanke akifanya cheers na mmoja wa makamanda wa jeshi la wanamaji kwenye hafla hiyo fupi iliyofanyika ndani ya meli ya kivita ya Ujerumani FGS Lübeck inayofanya doria ya kubaini maharamia kwenye pwani ya ukanda wa Bahari ya Hindi.

DSC_0017
Baadhi ya wanajeshi wa kikosi cha maji wa meli ya kivita ya Ujerumani FGS Lübeck kwenye hafla maalum ya kuwapongeza na kuwakaribisha nchini Tanzania iliyoandaliwa na ubalozi wa Ujerumani nchini Tanzania.

DSC_0022
Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Mh. Ali Davutoglu (kushoto) akibadilishana mawazo na mmoja wa maafisa wa bandari ya Dar es Salaam.

DSC_0029
Sehemu ya muonekano wa meli ya kivita ya ya Ujerumani FGS Lübeck wakati hafla ya kuupongeza msafara wa kikosi cha wanamaji wa jeshi la Ujerumani kilichoongozwa na Kamanda Peter Christian Semrau.
DSC_0030
Baadhi ya makanda wa kikosi cha wanamaji wa jeshi hilo wakilinda lango kuu la kuingia ndani ya meli hiyo.
DSC_0036
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya CFAO Motors, Bw.Wayne McIntosh (kushoto) akibadilishana mawazo na mmoja wanakikosi cha maji wa meli ya kivita ya ya Ujerumani FGS Lübeck iliyotia nanga kwenye bandari ya Dar es Salaam.
DSC_0038
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya CFAO Motors, Bw.Wayne McIntosh akihoji jambo kwa mmoja wa wanakikosi cha maji wa meli ya kivita ya ya Ujerumani FGS Lübeck ambaye jina lake halikuweza kufahamika kiurahisi.
DSC_0032
Pichani juu na chini ni baadhi ya wageni waalikwa wakibadilishana mawazo kwenye hafla hiyo.
DSC_0071
DSC_0065
Kamanda Peter Christian Semrau anayeongoza kikosi cha wanamaji wa meli ya kivita ya Ujerumani FGS Lübeck, inayofanya doria katika ukanda wa Bahari ya Hindi kama sehemu ya jeshi la kimataifa linaloendesha operesheni Atalanta akiwa kwenye picha ya pamoja na wageni waalikwa.
DSC_0057
Wageni waalikwa wakiendelea kupata picha ya kumbukumbu na Kamanda Peter Christian Semrau anayeongoza kikosi cha wanamaji wa meli ya kivita ya Ujerumani FGS Lübeck, inayofanya doria katika ukanda wa Bahari ya Hindi kama sehemu ya jeshi la kimataifa linaloendesha operesheni Atalanta kubabili maharamia.
DSC_0059
Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Mh. Egon Kochanke katika picha ya pamoja na Afisa wa kitengo cha habari Ubalozi huo, John Meirikion.
DSC_0069
Pichani ni baadhi ya wageni waalikwa wakipata picha ya pamoja ndani ya meli hiyo ya kivita.
DSC_0070
Afisa wa kitengo cha habari Ubalozi wa Ujerumani nchini Tanzania, John Meirikion akipata picha ya pamoja na mmoja wa wageni waalikwa ndani ya meli ya kivita ya Ujerumani FGS Lübeck iliyotia nanga bandari ya Dar es Salaam.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .