RAIS AWASILI KATIKA UWANJA WA UHURU KUONGOZA SHEREHE ZA UHURU
Posted in
Kitaifa
No comments
Tuesday, December 9, 2014
By
danielmjema.blogspot.com
Amiri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama Rais Jakaya Kikwete tayari amekwisha wasili katika uwanja wa Uhuru ambapo sherehe za miaka 53 zikiathimishwa hapo ambapo yeye ndiye mwenyeji wa sherehe hizo ambazo kwake niza mwisho katika uongozi wake.
Awali Rais alifika na kupanda jukwaa maalumu,ambapo uliimbwa wimbo wa taifa ukifuatiwa na upigaji wa mizinga 21, na baada ya hapo akafanya ukaguzi wa vikosi vya ulinzi na usalama.
Maadhimisho haya ya tanzania bara yanaathimishwa toka ilipojipatia uhuru toka kwa Muingereza Desemba 9, mwaka 1961.
Maadhimisho haya ya 53 ni muhimu kwa Watanzania, kutokana na kwamba nchi ipo katika kipindi cha uchaguzi, ambapo Watanzania siku ya Jumapili Desemba 14, watapiga kura, katika uchaguzi wa serikali za mitaa, vitongoji na vijiji.
Uchaguzi huo ni muhimu, kutokana na viongozi katika ngazi hiyo kuwa karibu kabisa na jamii.
Tanzania pia inaadhimisha miaka 53 ya uhuru wake ikiwa katika harakati za uchaguzi mkuu wa Rais na Wabunge unaotarajiwa kufanyika mwakani.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :