KUSHUKA KWA KIWANGO KUMPONZA NEYMAR, HII NDIYO KAMPENI CHAFU DHIDI YAKE
Posted in
Michezo
No comments
Wednesday, April 20, 2016
By
danielmjema.blogspot.com
Vyanzo hivyo habari vimetoa taarifa kwamba tabia ya Neymar kupenda kula sana bata, kusafiri bila ushari mzuri wa kitabibu, kwenda kufanya matangazo binafsi ya biashara, na mambo mengine kumepelekea kuathirika kwa kiwango chake. Vyanzo hivyo vya habari vinasema kwamba kumekuwepo na malalamiko kutoka ndani ya klabu kutokana na tabia hizo za nahodha huyo wa Brazil.
Taarifa za vyanzo hivi vya habari zinaonekana kutolewa na sehemu ya bodi ya wakurugenzi ambao wamekuwa wakikerwa na kiwango cha Neymar. Baadhi ya wajumbe hao pia wamekuwa wakishauri wenzao mshambuliaji huyo auzwe mwishoni mwa msimu kwa ada ya 190 million ambayo imetajwa kwenye mkataba katika kipengele cha kuvunja mkataba.
CHANZO: http://shaffihdauda.co.tz/
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :