MIAKA 11 TANGU KIFO CHAKE; JE AJALI YA HELIKOPTA ILIYOMUUA COL. JOHN GARANG ILIPANGWA AU ILIKUWA NI YA KAWAIDA?

No comments
Friday, April 15, 2016 By danielmjema.blogspot.com

Miaka 11 imepita sasa tangu kufariki kwa mwanzilishi wa kundi la waasi wa SPLM nchini Sudan, John Garang ambaye aliaga dunia katika ajali ya helikopta. Huku dunia ikiendelea kumkumbuka 'Komandoo' huyu aliyejitolea maisha yake, kwa ajili ya kuwakomboa wananchi wake wa Sudan Kusini.

Dunia inapoendelea kumkumbuka mwanamapinduzi huyu ambaye alishinda msituni kwa miaka mingi akipambana na serikali ya Sudan, ilikujitenga na kujitawala wenyewe. Swali la kujiuliza ni je kifo cha Garang kilisababishwa 'kilitengenezwa' au ni ajali ya kawaida? je, nani aliyemuua Garang? na kwanini?

Kifo cha John Garang kilipokelewa kwa uzuni mkubwa hususan mjini Khartoum ambako wafuasi wake waliamua kuingia mitaani na kuzusha machafuko, wakionekana dhahiri kutokubaliana na taarifa ya kifo cha mkombozi huyu, hii ilikuwa ni Agosti mosi, mwaka 2005.



 
Mara tu baada ya kifo chake kuthibitishwa rasmi, maelfu ya mashabiki wake waliingia bararani katika mji mkuu Khartoum katika maandamano yaliyokumbwa na machafuko. wakiwa na visu na vyuma, wafuasi wa John Garang, waliwapiga watu, kuyavunja maduka na magari na hata kuzichoma moto. yote haya ni kutokana na akili zao kama ilivyokuwa kwangu wakati huo, kutokubaliana na kiini cha Ajali ya Ndege iliyopelekea kifo chake.



Sio wafuasi wake tu walioshtushwa na kifo hicho, Viongozi kadhaa wakuu wa ulimwengu, walieleza masikitiko yao  ambapo katika taarifa yake, Rais Omar El Bashir ambaye alisaini makubaliano ya amani na Col. John Garang yapata wiki tatu kabla ya kifo chake, alikaririwa akisema anayo imani kubwa kuwa mpango wa amani utaendelea kutekelezwa kama ilivyopangwa.

Kwa upande wake Rais Salva Kiir Mayardit wa Sudan Kusini ambaye wakati huo alikuwa ni Naibu wa John Garang, alisema licha ya kuondoka kwa kiongozi wao, chama cha SPLM, kitaendelea na mozi na kuogeza kwamba watadumisha umoja na kuendeleza sera za kiongozi wao.

Waziri wa Uganda wa mambo ya kigeni (wakati huo) Sam Kutesa, aliitaja ajali hiyo iliyogharimu uhai wa Garang kuwa ni tukio baya, msiba mkubwa ambao umeikumba siyo tu Sudan bali pia kanda nzima. mwengine aliyeshtushwa na kifo hicho ni aliyekuwa Rais wa Kenya, Mwai Kibaki.

Kama kawaida baada ya vifo hivi vya utata, yamesemwa mengi ambapo mengine badala ya kutoa uelekeo wa ufumbuzi wa kitendawili kinachoandama chanzo cha vifo hivi, ni muendelezo wa taarifa 'pasua kichwa'. SAUTI KUU katika upekuzi wake, inajaribu kujibu swali moja kuu; nini chanzo cha kifo cha Col. John Garang?


Mnamo Julai, 30, mwaka 2005, Mtaalamu wa mitambo ya mawasiliano (Switchboard Technician) katika Afisi za kampuni ya mawasilianoya MTN, mjini Kampala, Andrew Ndawula aliripotiwa kutoweka katika mazingira tatanishi.

Jioni moja akiwa anatoka kazini, Ndawula alidaiwa kupotea katika mazingira tatanishi na hajaonekana tena tangu wakati huo. Kwa mujibu wa taarifa za kusadikika, mtaalamu huyu alitoweka usiku wa Julai30, mwaka 2005, ikiwa ni siku moja kabla ya Ajali ya Chopa iliyosababisha kifo cha Makamu huyo wa Rais wa Sudan

Inasemekana kwamba, Ndawula kabla ya kutoweka, alifanikiwa kusikia mazungumzo fulani ya 'watu fulani' ambao wanadaiwa kuwa ni viongozi wakuu wa Serikali wakijadili mpango wa mauaji ya Garang.
Madai haya yanayohusisha kutoweka kwa mtaalamu huyu (Ndawula) na kifo cha Garang yanaweza yakawa na ukweli ndani yake, kwa sababu siku ya tukio la ajali ya Chopa iliyombeba Garang (ambayo ilikuwa ni ya Rais Museveni), mtandao wa simu wa MTN, ulikuwa na matatizo ya mawasiliano, ambapo hakukuwa na simu iliyokuwa ikiingia wala kutoka na wala haikuwa rahisi kutuma ujumbe mfupi 'SMS' -hakukuwa na mawasiliano.

Ikumbukwe pia kuwa, moja ya sababu iliyotolewa na serikali ya Museveni ni kuwepo kwa tatizo la mawasiliano na usahidi zaidi wa madai haya ni kwamba, inasemekana usiku huo, Andrew Ndawula aliwasikia wenzake wakijadiliana na Waziri wa Mawasiliano wa wakati huo, Dr James Nsaba Buturo kuhusu mpango wa kuzima mitambo ya mawasiliano ya MTN na baada ya kugundua kuwa siri yao sio siri tena, waliamua 'kumpoteza' Ndawula.

Pia baada ya kutweka kwa Ndawula, Mama yake Mzazi alidaiwa kuliomba Jeshi la Polisi pamoja na kampuni ya MTN, wamsaidie kumpata mwanae lakini walimpuuza jambo linazidi kuzua utata na kufanya madai ya mpango wa kuuwawa kwa Garang kusukwa na Serikali ya Museveni yaonekane kuwa ya kweli.

Hata hivyo, kuna kila dalili ya kwamba kiongozi huyo wa zamani wa SPLM, aliuwawa, lakini swala ambalo bado haliko wazi ni kama kweli Garang aliuwawa, je ni nani hasa aliyemuua Garang na kwanini huyo muuaji aliamua kuyakatisha Uhai wake mara tu baada ya kufanikisha na Amani?

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .