SERIKALI YA KENYATTA IMETUMIA BILIONI 4 KWA AJILI YA SAFARI, NDANI YA MIEZI SITA

No comments
Friday, April 15, 2016 By danielmjema.blogspot.com


RIPOTI ya mkaguzi na msimamizi wa bajeti ya serikali, nchini Kenya inaonesha kwamba safari za Rais Uhuru Kenyatta, Makamu wake William Ruto pamoja na baadhi ya maafisa waandamizi wakuu wa Serikali, walitumia takribani shilingi bilioni 4 katika Safari za ndani na nje ya nchi, katika kipindi cha miezi sita pekee.




Ripoti hiyo iliyofanywa katika kipindi kati ya mwezi Julai hadi Desemba, mwaka 2015, ilionesha kuwa Safari za ndani iliigharimu Serikali jumla ya shilingi bilioni 2.5 huku Safari za nje ya nchi ikitumia takribani shilingi bilioni 1.5 na kufanya matumizi kwa ajili ya Safari kufikia kiasi cha shilingi bilioni 4.

Ripoti hiyo pia inaonesha kuwa Serikali ilitumia shilingi bilioni 123.7 kwa ajili ya matumizi binafsi ambayo ni sawa na asilimia 46.3 ya jumla kuu ya matumizi ikiwa ni ongezeko la matumizi kutoka shilingi bilioni 123.1 iliyoripotiwa katika nusu ya kwanza ya matumizi ya bajeti ya Serikali kuu, mwaka 2014/15.


Idara ya Bunge la Taifa, hata hivyo iliandikisha kiwango kikubwa cha matumizi kwa ajili ya safari za ndani ambayo ni 865 milioni huku Wizara ya Mambo ya Nje na Biashara za kimataifa ikiandikisha kiwango cha juu cha matumizi cha shilingi 732.5 milioni.

Ofisi ya Rais, ilitumia shilingi 208.1 milioni kwa ajili ya Safari za ndani na shilingi 111.2 milioni katika kughramia safari za nje ambayo ilikuwa ni kwa wote, Kenyatta na Ruto na kufanya matumizi ya jumla kwa ajili ya Safari tu kwa ajili ya viongozi hao kufikia shilingi 319.3 milioni.

Ofisi ya Rais pia ilitumia shilingi 617 milioni kwa ajili ya shughuli ya kukirimu wageni, ambayo ni sehemu ya shilingi 1.7 bilioni iliyotumika katika idara zote za serikali nchi nzima. Upande wa Upinzani ukiongozwa na Waziri mkuu wa zamani, Raila Odinga imekuwa ikilalalmikia safari za mara kwa mara ya Rais Kenyatta na Naibu wake, William Ruto.

“Kuna watu wanaoandamana na Rais katika ziara zake, kwa ajili ya kwenda kufanya 'shopping', Rais wa Tanzania John Magufuli, alipiga marufuku safari za nje nchini mwake na kup[unguza idadi ya watu wanaoandamana na Rais katika misafara yake, nadhani ni muda mwafaka na sisi tuige kutoka kwa Magufuli," alisema Raila katika moja ya Hotuba zake hivi karibuni.

Taarifa zinaonesha kwamba hadi kufikia Desemba 2015, Rais Kenyatta tayari alishafanya ziara 43 katika katika kipindi cha miaka mitatu akiwa madarakani huku mtangulizi wake, Mwai Kibaki yeye Ripoti ikionesha kuwa alifanya Ziara 13 tu ndani ya kipndi cha miaka 10 ya utawala wake.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .