MAGUFULI AMFUTA KAZI MHARIRI WA MAGAZETI YA SERIKALI-TANZANIA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
ametengua uteuzi wa Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali (TSN) Bw.
Gabriel Nderumaki.
Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Mhandisi John Kijazi, iliyotolewa jana, Aprili 14, 2016, kwenda kwa vyombo vya Habari, kupitia Ofisi ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu ya Tanzania, nafasi ya Nderumaki itakaimia na Bi. Tuma Abdallah, ambaye amekuwa mhariri mtendaji msaidizi wa magazeti ya serikali (TSN).
Taarifa hiyo ilisema kuwa uteuzi wa Nderumaki ulitenguliwa kuanzia tarehe 18 Machi, 2016. Hakuna maelezo yoyote zaidi yaliyotolewa kuhusu sababu za kutenguliwa kwa uteuzi wa Bw Nderumaki. TSN huchapisha magazeti ya Daily News, Sunday News, Habari Leo Jumapili na Spoti Leo.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :