MFANYABIASHARA AICHANGIA TAASISI YA RAIS MSTAAFU WA TANZANIA TSH.210 MILIONI
Posted in
afrika mashariki
No comments
Friday, April 15, 2016
By
danielmjema.blogspot.com
Mwanzilishi wa Taasisi ya Mkapa (Mkapa
Foundation), Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mh. Benjamin William Mkapa
(kushoto), mgeni rasmi Rais na Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya Mohammed
Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group), Mohammed Dewji (kulia) pamoja
na Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini ya Mkapa Foundation, Balozi Charles
Sanga wakiwasili katika sherehe za miaka 10 ya Mkapa Foundation
zilioambatana na harambe ya kutunisha mfuko wa taasisi hiyo
zilizofanyika kwenye ukumbi wa Golden Jubilee Tower. (Picha na Zainul
Mzige)
Na Zainul Mzige, Dar es salaam
Mfanyabiashara mkubwa nchini Tanzania, Mohammed Dewjia ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya
Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group), Mohammed Dewji
ameuchangia mfuko wa Taasisi ya Benjamin William Mkapa (Mkapa
Foundation), Milioni 210 ili kuiwezesha kuzidi kutoa huduma bora kwa
jamii.
Mohammed Dewji |
Mohammed Dewji ametoa kiasi hicho cha
pesa akiwa kama mgeni rasmi katika sherehe za kutimiza miaka 10 tangu
kuanzishwa kwa Taasisi ya Benjamini Mkapa (Mkapa Foundation) ambapo
Milioni 200 imetolewa na Taasisi ya Mohammed Dewji (Mo Dewji Foundation)
na Milioni 10 imetolewa na MeTL Group.
Akitoa hotuba katika sherehe hiyo,
Mohammed Dewji amesema kuwa ametoa msaada huo ili kuiongezea nguvu
Taasisi ya Benjamin Mkapa (Mkapa Foundation) katika kutoa huduma
mbalimbali kwa jamii ya Watanzania.
Alisema kuna changamoto nyingi nchini
ambazo zimekuwa zikijitokeza na ili kukabiliana nazo zinahitajika
taasisi kama ya Benjamin Mkapa ili ziweze kusaidiana na Serikali na ili
waweze kutatua changamoto hizo zinahitajika sekta binafsi kusaidiana nao
kukabili changamoto hizo.
“Nimekuwa mstari wa mbele kusaidia sehemu
ambazo zinaonekana kuwa na mahitaji na changamoto nchini zipo nyingi
haina jinsi inabidi kushirikiana ili kupambana na changamoto hizo,”
alisema Dewji.
Aidha Dewji aliyataka mashirika binafsi mengine kuungana kwa pamoja na
kusaidia kumaliza changamoto zilizopo nchini kwani anaamini kuwa wana
nafasi kubwa kukabiliana na matatizo hayo na kuweza kuyamaliza.
Nae mwanzilishi wa Taasisi ya Mkapa
(Mkapa Foundation), Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mh. Benjamin William
Mkapa alimshukuru Mohammed Dewji kwa msaada ambao amewapatia na anaamini
ni mmoja wa watu wa kuigwa nchini kutokana na misaada ambayo amekuwa
akiitoa nchini kwa kupitia taasisi yake ya Mohammed Dewji (Mo Dewji
Foundation).
“Mohammed Dewji ni mfano wa kuigwa nchini
na ameweza kuboresha biashara ya Tanzania kimataifa, ninaamini utadumu
kwa kipindi kirefu zaidi na kuwa balozi mzuri wa Tanzania,” alisema
Mkapa.
Katika sherehe hizo za kuadhimisha miaka
10 tangu kuanzishwa kwa Taasisi ya Benjamin William Mkapa, kulifanyika
harambee ambapo jumla ya Bilioni moja na Milioni mia moja na sabini
zilichangishwa.
Mgeni rasmi Rais na Mkurugenzi Mkuu wa
Makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group),
Mohammed Dewji (kushoto) akimkabidhi zawadi ya picha iliyoandaliwa na
wafanyakazi pamoja na bodi ya Mkapa Foundation, Mwanzilishi wa taasisi
ya Mkapa, Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mh. Benjamin William Mkapa
wakati wa sherehe za miaka 10 ya taasisi hiyo zilizoambatana na harambee
ya kutunisha mfuko wa taasisi hiyo ambapo jumla ya shilingi bilioni
moja na milioni mia moja sabini zilichangishwa.
Mohammed Dewji (kushoto) akimkabidhi tuzo Mwanzilishi wa taasisi ya
Mkapa, Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mh. Benjamin William Mkapa ya
kutambua mchango wake wa kuleta matumaini kwa watu wenye mahitaji na
kuthamini maono na muongozo kama mwanzilishi wa taasisi ya hiyo
iliyoanzishwa mwaka 2006 kwenye sherehe za miaka 10 ya taasisi hiyo
iiliyoambatana na hafla ya harambee kwa ajili ya kuchangia taasisi hiyo.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :