UNATUMIA 'SMARTPHONE' ? JE, UNAIJUA SIMU YAKO? HAYA HAPA MAMBO YA KUJIFUNZA KUHUSU SMARTPHONE'
Posted in
No comments
Sunday, April 17, 2016
By
danielmjema.blogspot.com
MATUMIZI ya simu za kisasa (smartphone) yamezua maneno na uvumi wa kila aina katika blogu, magazeti mbalimbali, barua-pepe, mitandao ya WhatsApp na Facebook, hata hivyo, mtumiaji wa simu hizi hatakiwi kuamini kila kitu anachokiona mitandaoni. Siri, au mambo muhimu kuhusiana na simu za aina hiyo ni hizi zifuatazo:
Siri ya 1: Mifumo ya
kisasa ya mawasiliano na ya kuongoza ndege ni yenye utaalamu wa hali ya
juu. Hivyo, hata kama ndege itakuwa ina watu wengi walio na imejaa simu
za mkononi kiasi gani simu hizo haziwezi kuathiri mifumo hiyo ya
mawasiliano katika ndege hiyo.
Siri ya 2:
Petroli hulipuka au husika moto kirahisi hata kwa cheche tu. Cheche
inaweza ikatoka katika viberiti, vidude vya kuwashia sigara au hata
umeme, lakini si kutoka katika simu ya mkononi. Wasiwasi uliopo kwamba
simu mbovu au hata betri yake inaweza kutoa cheche au moto ni jambo
ambalo haliwezekani na hapana tukio lolote lililothibitishwa kutokana na
dhana hiyo.
Siri 3: Vyombo vyote vya
elektroniki ambavyo vina betri ambazo baada ya muda hulazimika
kuchajiwa, vina mifumo ya ndani kwa ndani ya usalama inayozuia nguvu ya
umeme kuzidi na hivyo kuleta madhara. Mara tu betri inayochajiwa
ikifikia kiwango chake kinachotakiwa, simu hiyo itaacha yenyewe kupokea
umeme, licha ya kwamba mashine ya kuchajia inaweza, katika matukio
kadhaa, ikaendelea kupokea umeme kidogo.
Siri ya 4: Chombo chochote
kinachotumia betri kama vile simu ya mkononi au kompyuta-mpakatol,
uwezo wa betri yake unahusiana na muundo au utendaji kazi wa mashine
husika. Hivyo, ukiwa na simu mbili zinazofanana za mkononi, ile ambayo
inakaa zaidi kwenye chaja ni ile ambayo ina kiwambo na vikorombwezo
vingi zaidi vya kielektroniki.
Siri ya 5: Mifumo mingi ya kufungulia kurasa kwenye simu (browsers) inatumika kutunza kumbukumbu ya mtumiaji wakati anatumia.
Siri ya 6: Ni kweli
kumekuwepo matukio machache ya simu za mkononi kulipuka, lakini ukweli
ni kwamba ni betri ndizo husababisha moto na kulipuka, na si simu
zenyewe.
Siri ya 7: Simu yoyote
bora kutoka katika kampuni yoyote maarufu lazima ifanyiwe jaribio la
kuhakikisha kwamba simu hiyo haitatoa mionzi mingi kiasi cha kuweza
kusababisha madhara. Jaribio hilo huitwa Specific Absorption Rating –
SAR.
Source: GPL
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :