WATU 100 WAHOFIWA KUTEKETEA KATIKA HEKALU LA WAHINDU, WENGINE 150 WAMEJERUHIWA

Posted in
No comments
Sunday, April 10, 2016 By danielmjema.blogspot.com

Taarifa zilizotufikia hivi punde ambazo zimethibitishwa na Polisi nchini India, zinasema kuwa Takribani watu  zaidi ya watu 100 wameuawa na wengine 150 kujeruhiwa katika moto uliotokea katika hekalu la Wahindu katika jimbo la Kusini la Kerala.



 Moto huo uliotokea katika wilaya ya Kollam ulianza wakati wa sherehe ya mapema asubuhi. Polisi wanasema huenda moto huo ulianzishwa na fataki. Waziri wa mashauri ya nchini katika jimbo la Kerala, Ramesh Chentallah, alisema kuwa uchunguzi wa mahakama utaanzishwa.

Waziri wa Mashauri ya Ndani, Oommen Chandi, na bwana Ramesh wamesema kuwa watatembelea eneo hilo. Polisi wamesema kuwa moto huo umedhibitiwa lakini shughuli za uokozi zingali zinaendelea. Maelfu ya waumini walikuwa wamekongamana ilikushuhudia maonesha haya ya kila mwaka ya fataki.


Uchunguzi wa kwanza umebaini kuwa maafisa wakuu katika eneo hilo waliwanyima waratibu wa maonesho hayo leseni ya kuandaa maonesho ya fataki kufuatia hofu kuhusu usalama wa umma. Waziri mkuu wa India bwana Narendra Modi amewasili Kerala.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .