Okumbi aweka wazi Jeshi litakaloikabili Tanzania leo, Ochomo anaanzia benchi

Posted in
No comments
Sunday, May 29, 2016 By danielmjema.blogspot.com

KOCHA mkuu wa timu ya Taifa, Harambee Stars, Stanley Okumbi, ametaja kikosi cha jeshi lake litakalo shuka dimbani, kuchuana na timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars huku mshambuliaji hatari wa Muhoroni Youth, ambaye ni kinara wa mabao katika Ligi kuu ya Kenya, msimu wa 2016/2017 inayoendelea kutimua vumbi, Wycliff Ochomo (Mabao 11) akianzia Benchi.
Katika kikosi hicho pia yupo bek hatari wa kushoto kutoka klabu ya Gor Mahia, Eric Ouma 'Marcelo'. Marcelo mwenye umri wa miaka 19 pekee ni mmoja wa wachezaji muhimu katika kikosi cha Kogalo msimu huu, lakini kama mwenzake (Ochomo) naye ataanzia benchi.
Wycliffe Ochomo katika moja ya matukio uwanjani
Kinara wa mabao katika ligi ya Zambia, anayekipiga na Zesco United, Jesse Were (mabao 10) anatarajiwa kuongoza safu ya mashambulizi. Eneo la Difensi inashuhudia Aboud Omar anayekipiga nchini Bulgaria na Eugene Asike (Tusker) wakirejea kikosini kusimamia idara ya ulinzi huku Nahodha Victor Wanyama (Southampton), Anthony Akumu na Humphrey Mieno wakiunda safu ya kiungo (Mid-field)
Aidha katika kikosi hicho cha Okumbi kitakuwa na Wachezaji wawili ambao watakuwa na jukumu ya kukimbia katika viungo vya pembeni (Wings). mawinga hao ni Eric Johanna (Mathare United) na Ayub Timbe anayesakata kabumbu katika klabu ya Lierse (Belgium). 
Kikosi cha kwanza:
Boniface Oluoch, Joackins Atudo, Aboud Omar, Eugene Asike, David Owino, Anthony Akumu, Victor Wanyama, Ayub Timbe, Humphrey Mieno, Eric Johanna na Jackson Were
Wachezaji wa Akiba:
David Okello,Eric Ouma Otieno, Musa Mohamed, Ali Abondo, Wycliffe Ochomo, Mark Makwata na Cliffton Miheso.
Harambee Stars itamenyana na Taifa Stars leo, kuanzia saa 10:00 alasiri, majira ya afrika Mashariki, katika uwanja wa Moi Kasarani, jijini Nairobi.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .