Madiwani kutoka Kahama, nchini Tanzania waupongeza mgodi wa Buzwagi.
Posted in
afrika mashariki
No comments
Friday, June 3, 2016
By
danielmjema.blogspot.com
Afisa
mazingira wa Mgodi wa Buzwagi Bwana Lusajo Njobelo akifafanua jambo kwa
waheshimiwa madiwani na mbunge wa Kahama mjini Jumanne Kishimba
wakati wa ziara hiyo.
Na Dixon Busagaga
Madiwani
wa halmashauri ya mji wa Kahama wameupongeza Mgodi wa Dhahabu wa
Buzwagi ulioko wilayani Kahama mkoani Shinyanga, kwa
namna ambavyo umekuwa ukishiriki katika kutekeleza miradi mbalimbali ya
Maendeleo ambayo imekuwa na manufaa makubwa kwa wananchi wa Kahama na
hususuani vijiji vinavyozunguka Mgodi huo.
Pongezi hizo zimetolewa kwa niaba ya madiwani hao na mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Kahama Abeli Shija wakati wa ziara ya
siku moja iliyokuwa imelenga kujionea namna Mgodi huo unavyofanya shughuli zake za uchimbaji.
“Kwa
niaba ya halmashauri ya mji tunawapongezeni sana kwa namna ambavyo
mmekuwa chachu ya mendeleo kwa wilaya yetu na tunafarijika
kwa sababu leo mji wetu uko na barabara nzuri lakini pia wakazi wa
Mwendakulima na maeneo ya jirani wanao uhakika wa kupata huduma nzuri za
afya katika kituo cha afya ambacho mmeshiriki kukijenga, watoto wetu
pia wanaouhakika wa kusoma vizuri kutoka na miundo
mbinu mlioiweka katika baadhi ya shule na hasa ujenzi wa maabara za
kisasa ” alisema Shija.
Mwenyekiti
huyo pia aliuomba uongozi wa Mgodi kuwezesha upatikanaji wa kifaa
kitakachosaidia mji wa Kahama kupata umeme wa uhakika
ambao utaendana na Mahitaji ya shughuli za kiuchumi kwa mji wa Kahama
kutokana na line iliyopo sasa kushindwa kukizi Mahitaji ya wakazi wa mji
wa huo.
Akijibu
ombi hilo Meneja mkuu wa Mgodi wa Buzwagi mhandisi Asa Mwaipopo amesema
mpaka sasa kifaa hicho kimeisha fika na kinachosubiliwa
ni wataalamu waliotengeneza kifaa hicho kutoka ujerumani kuja na
kukifunga.
“Kifaa
kimeisha fika na tunachosubiri kwa sasa ni wataalamu tu kuja na
kukifunga, matumaini yetu ni kuwa kazi hiyo itakapokamilika
wananchi wa Kahama wataondokana na tatizo la umeme usiokuwa wa
uhakika.” Alisema Mwaipopo.
Ziara
hiyo ambayo ilihusisha madiwani wa mji wa Kahama, Mbunge wa Kahama
mjini, Jumanne Kishimba na wataalamu wa halmashauri hiyo,
walipata fursa ya kutembelea maeneo mbali ya Mgodi huo na kuelezewa
namna suala la usalama wa mazingira linavyozingatiwa, ambapo madiwani
hao walishangazwa na namna Mgodi huo ulivyozingatia sheria mbalimbali za
mazingira na uchimbaji na kulifanya eneo hilo
kuwa salama zaidi.
Madiwani hao waliomba mgodi huo kuongeza
ufahamu kwa Jamii kwa kuongeza ziara nyingi zitakazo husisha wananchi wa
kawaida kwa lengo la kuwafahamisha shughuli zinazofanywa na Mgodi hali
ambayo wamesema itasaidia kupunguza taarifa
za uongo ambazo zimekuwa zikisambaa mitaani kutokana na Jamii kutokujua
ukweli.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :