Will Smith na Lenox Lewis kuwa mmoja wa wabebaji wa Jeneza la Mohammad Ali

Posted in
No comments
Tuesday, June 7, 2016 By danielmjema.blogspot.com

Will Smith (kulia) kwenye filamu aliyoigiza maisha ya Muhammad Ali
Staa wa filamu nchini Marekani, Will Smith na bingwa wa ngumi wa dunia, Lennox Lewis wameteuliwa kuwa miongoni mwa watu watakaobeba jeneza la marehemu Muhammad Ali siku ya mazishi.

Familia ya marehemu Muhammad Ali imewateuwa wawili hao ikiwa Smith ni rafiki wa karibu wa familia hiyo tangu mwaka 2001 alipoigiza filamu ya iliyokuwa inamhusu marehemu Ali.


Bondia Lenox Lewix akiwa na Marehemu Mohammad Ali
Kwa upande Lewis ameteuliwa akiwa ni mmoja kati ya mabondia watatu waliowahi kuchukua ubingwa wa dunia mara tatu akiwemo na marehemu Ali.

Muhammad Ali alifariki Juni 4 kwenye hospitali ya huko Phoenix ambako alikuwa akitibiwa kutokana na matatizo ya kupumua na mazishi yake yanatarajiwa kufanyika Ijumaa hii huko Kentucky.
Will Smith akiwa katika picha na Mohammad Ali

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .