Mbunge wa Uganda agoma kupongezana na Spika Mteule
Posted in
No comments
Wednesday, June 6, 2012
By
danielmjema.blogspot.com
Spika wa Bunge la EALA Margaret Banbtonbg Zziwa
Kati
Hali isiyokuwa ya kawaida ndani ya Bunge la Afrika Mashariki (EALA) hii
leo wakati Wabunge hao wakiendelea kuapa, aliyekuwa Mgombea wa Kiti cha
Spika kutoka Uganda, Mwanasheria Dora Byamukama (40) amegoma
kumkumbatia (hug) Spika Mteule wa Bunge hilo ambaye pia anatoka nchini Uganda, Spika Margaret Banbtonbg Zziwa (49).
Ilikuwa
ni kawaida ya wabunge wote waliokuwa wakiapa kukumbatiana au kupeana
mikono ya pongezi na Spika huyo lakini Mbunge huyo aliyeanguka katika
Uchaguzi wa Spika kuzira kufanya hivyo jambo lililozua mguno ndani ya
Bunge na kwa wageni waalikwa kukumbwa na butwaa.
Safari
hii ni zamu ya Uganda kuchukua kiti cha Spika baada ya Tanzania na
Kenya kushika nafasi hiyo katika Bunge la Awamu ya Kwanza na Pili.
Bunge hilo limezinduliwa leo na wabunge wake wakiendela kuapa hivi sasa katika Ukumbi wa Mikutano wa AICC jijini Arusha.
Zziwa
ambaye ni Mchumi kitaaluma amemshinda mwanamke mwingine kutoka Uganda,
Mwanasheria Dora Byamukama (40) baada ya uchaguzi huo kurudiwa mara
mbili baada ya kura za awali kutokufikia idadi asiliamia 30 inayotakiwa
ya wapiga kura wote.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :