KUAMBIANA KUZIKWA JUMANNE JIJINI DAR ES SALAAM...
Posted in
Kifo
No comments
Sunday, May 18, 2014
By
danielmjema.blogspot.com
MSAANI maarufu, Adam Philip "COCO" Kuambiana aliyefariki ghafla jana jijini Dar es salaam, anatarajiwa kuzikwa keshokutwa Jumanne katika Makaburi ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam, huku mazishi yake yakitanguliwa na shughuli ya kumuaga katika Viwanja vya Leaders Club, saa 2 kamili asubuhi.
Kuambiana
aliyetamba na filamu kadhaa, ikiwamo ile ya Regina iliyotungwa na msanii Jacob
Stephen JB, alifariki janawakati anawahishwa katika Hospitali ya Mama
Ngoma Mwenge, jijini Dar es Salaam baada ya kuanguka ghafala akiwa Location katika Hoteli ya Silver Rado iliyopo Sinza kwa Remmy.
Akizungumza jana mchana, jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Maafa na Sherehe wa Chama Cha Waigizaji mkoani Dar es Salaam, Kaftany Masoud, alisema taratibu za mazishi yake zitaanza kwa kuagwa Leaders Club.
Katika hatua nyingine, msanii wa maigizo na filamu, anayejulikana kwa jina la Ridhiwan Masoud, amefariki leo mchana katika Hospitali ya Taifa, Muhimbili, hivyo kuendeleza wimbi la misiba ya wasanii na wanamuziki Tanzania, ukiwamo msiba wa Amina Ngaluma, mwanamuziki wa dansi, ambaye jumanne na Jumatano mwili wake utaletwa Tanzania tayari kwa masishi yake.
Msiba wa msanii huyo upo maeneo ya Magomeni Mapipa, mtaa wa Mkadini, ambapo ndipo zitakavyoendelea taratibu za mazishi yake.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :