JERRY SILAA AIFAGILIA MeTL GROUP.
No comments
Tuesday, July 8, 2014
By
danielmjema.blogspot.com
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa akiwasili kwenye maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yanayoendelea katika viwanja vya maonesho vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar.
Na Mwandishi wetu
Mstahiki Meya wa manispaa ya Ilala, Jerry Silaa ameipongeza makampuni yaliyochini ya Kundi la METL kwa kuhakikisha ajira kwa watanzania na soko la mali ghafi kwa wakulima wa bidhaa mbalimbali nchini.
Silaa alisema hayo jana wakati alipotembelea banda la METL na kujionea bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na makampuni yake mbalimbali zikiwemo bidhaa za michikichi na katani.
Alisema kwa kutengeneza sabuni, mafuta na mali ghafi nyingine kutokana na michikichi kampuni za Metl zinawezesha wakulima kujiendeleza na pia kuwa na uhakika wa soko.
METL yenye makampuni zaidi ya 25 sehemu kubwa ya bidhaa zake zinatokana na mali ghafi inayozalishwa nchini na nyingine ni zile zinazotumika kwa ajili ya wakulima kama matrekta.
Aidha katika banda hilo kubwa ambapo kulijaa aina mbalimbali ya bidhaa kuanzia Sabuni,Vitenge, mafuta ya Mawese,vinywaji baridi, Matrekta na bidhaa za nyumbani, Mstahiki meya huyo alichezesha bahati nasibu za watu waliotembelea banda hilo.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa akisaini kitabu cha wageni kwenye ofisi za Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania, TANTRADE kwenye viwanja vya maonesho ya Sabasaba mara baada ya kuwasili.
Akizungumzia uwekezaji wa METL, Silaa alisema kwamba anafarijika na jinsi bidhaa za kampuni hizo zinavyoimarika ubora kila mwaka na kusema wakati umefika kwa serikali kuangalia wawekezaji wazawa.
Alisema kwa maoni yake serikali ione jinsi ya kuwasaidia wawekezaji wanaoagiza mitambo toka nje ili kodi wanaoyotakiwa kulipa wailipe baada ya kuanza kazi za uzalishaji.
“Hii itasaidia sana kuwa na wawekezaji wa ndani ambao wataweza kutoa huduma kama soko la mali ghjafi na pia kuongeza thamani ya bidhaa zinazoalishwa kutoka Tanzania” alisema silaa.
Aidha Silaa alipongeza MeTL Group kwa kuweza kutoa ajira kwa watanzania wazawa huku bidhaa zake nyingi zikiwa kimbilio la watanzania wote, hasa wa kipato cha chini.
Afisa Mwandamizi wa TANTRADE, Fidelis Mugenye, (kushoto) akimuonyesha Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa ratiba ya ziara kwenye mabanda mbalimbali ya maonesho ya Sabasaba yanayokaribia kufikia ukingoni.
“Naipongeza MeTL Group, kwa kuzalisha bidhaa bora ambazo ni kimbilio la wananchi wengi… hasa bidhaa zake za mafuta, sabuni, unga, vinywaji na bidhaa zingine kibao” alisema Silaa
Pia aliipongeza MeTL kwa upande wa kutoa ajira na kukuza uchumi hapa nchini, ikiwemo kuzalisha bidhaa nyingi na zenye ubora ikiwemo za kamba ya mkonge ambayo alisema ni majibu ya utunzaji wa mazingira kutokana na vifungashio vya plastiki kuwa chanzo cha uharibifu wa mazingira.
Katika bahati nasibu iliyochezeshwa mkazi wa Kijitonyama Jijiji Dar es Salaam, Irene Manamba amejishindia zawadi ya pikipiki mpya.
Aidha, katika droo hiyo, washindi wengine waliojishindia zawadi mbalimbali katika droo hiyo majina yao na wanakotoka ni Victoria Charles ambaye alikuwa mshindi wa pili mkazi wa Temeke, Julius Kamele (Tabata), Irene Mushi (Kijitonyama), Semi Anderson ((Dar es Salaam), Happyness Kalokola (Kitunda), Noel Kalenga (Sinza Kumekucha), Adam Mkwaya (Mabibo), Mery Msangi (Dar es Salaam) na Aisha Abeid (Tabata).
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa akisalimiana na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa ndani ya ofisi za Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania, TANTRADE.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :