KUMBE! Mafanikio ya Rapa 50 Cent yanatokana na Kulelewa Bibi yake (Grandmother)

Posted in
No comments
Thursday, May 12, 2016 By danielmjema.blogspot.com

Ukitazama hiyo picha hapo (kulia), utamuona 50 Cent na bibi yake, Beulah Jackson.. ngoja nikusimulie kisa kidogo cha wawili hawa. Akiwa na miaka mitano, 50 Cent alilelewa na bibi yake Beulah Jackson baada ya mama yake Sabrina kufariki kwa kuzidiwa na madawa ya kulevya aliyowekewa kwenye kinywaji. Kwenye nyumba hiyo, bibi alikuwa akilea wajukuu wengine 9.


Kumbuka marehemu Sabrina alikuwa muuzaji wa madawa ya kulevya na alimzaa 50 Cent akiwa na miaka 15 tu. Chini ya ulezi wa bibi, 50 Akawa mtoto wa mitaani, na alipofika miaka 12 akaanza kujihusisha na biashara ya kuuza madawa ya kulevya ili apate hela ya kujikumu kimaisha. Miaka mitatu baadae (akiwa na miaka 15) 50 Cent akawa muuzaji mkubwa wa madawa hayo kwenye mtaa wao hali iliyomfanya aache shule.

50 Cent anasema kuwa bibi yake alishawahi kumwambia umasikini ndio ulimfanya marehemu mama yake muhuni, na asingependa mjukuu wake arithi kazi hiyo. Alitamani asome ili aje kuwa na kazi ya maana. Lakini mwisho wa siku 50 alijiingiza kwenye uuzaji wa madawa, mpaka alipokamatwa na polisi na kupelekwa kwenye kambi ya jeshi kwa ajili ya mateso yaliyodumu kwa miezi sita.


 Alipotoka huko, aliamua rasmi kuachana na madawa na kuanza kuimba kwani hakupenda kuendelea kumkosea bibi yake. Leo 50 Cent ni rapa mkubwa duniani, ana utajiri zaidi ya dola mil 150, Lakini bibi yake hayupo tena duniani, ameshafariki. 50 Cent ameendelea kumshukuru bibi yake kwa kubadili maisha yake.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .