Mashabiki wa Eskisehirspor ya Uturuki wachoma uwanja moto kutokana na kukerwa na timu yao kufungwa
Posted in
Michezo
No comments
Monday, May 16, 2016
By
danielmjema.blogspot.com
Mashabiki wa soka nchini Uturuki wameishangaza Dunia baada ya kuamua kuchoma uwanja moto. Mashabiki wa klabu ya Eskişehirspor wameamua kuchoma uwanja wao baada ya timu yao kufungwa goli dakika ya 93, kipigo ambacho kimefanya kuwa katika nafasi ya kushuka daraja.
Mchezo huo uliomalizika kwa Eskişehirspor kufungwa goli 2-1, mashabiki walivamia uwanja wao na kuanza kuchoma moto, Eskişehirspor msimu ujao huenda ikashiriki Ligi daraja la pili Uturuki, kutokana na kuwa nafasi mbaya katika msimamo wa Ligi KuuUturuki.
Tizama Video ya Mashabiki hao walivyochoma uwanja wao Moto
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :