Vin Diesel amezungumza haya kuhusu Paul Walker (Marehemu), Fast & Furious 8 ikianza kutengenezwa
Posted in
Burudani
No comments
Monday, May 23, 2016
By
danielmjema.blogspot.com
Staa wa Fast & Furious, Vin Diesel amemkumbuka marehemu rafiki yake Paul Walker kwenye post ya Instagram aliyoandika Jumamosi, May 21 wakati filamu mpya ya The Fast and the Furious ikianza kutengenezwa.
“Many of the crew members who have worked on several of the past Fast films are here again to help us make something special,” Diesel, 48, aliandika kwenye picha yake na Walker, aliyefariki kwa ajali ya gari November 2013 akiwa na miaka 40.
“One of them at the end of the week came up to me and said wow what we are capturing on film is excellent… And then looked at me and said Paul would be proud. #wemakethemwithourhearts,” aliongeza. Walker alifariki kipindi Furious 7 inakaribia kukamilika.
Tyrese Gibson, Ludacris, Dwayne “The Rock” Johnson na Michelle Rodriguez, wanarejea kwenye Fast 8, huku wakiongezeka Scott Eastwood na Charlize Theron.
Universal Pictures walionjesha kwenye Instagram picha ya kwanza ya Theron atakayecheza kama adui kwenye filamu hiyo akiitwa Cipher. Fast 8 inatarajiwa kutoka April 14 mwakani.
Habari Zingine
- Timbulo: SIjarejea kwenye ualimu
- Vijana wazidi kujitokeza usaili wa Maisha Plus East Africa, Dar es salaam yatia fora
- RAPPER WA CAMEROON, NGOMA AACHIA VIDEO YA WIMBO MPYA ‘ALL LES DAY’, AIELEZEA COLLABO YAKE NA RAY VANNY
- New Hit: Lady Jay Dee – Sawa Na Wao
- Madonna atembelea makazi duni ya Kibera, Nairobi
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :