Showing posts with label Ulimbwende. Show all posts
Showing posts with label Ulimbwende. Show all posts

MISS SINGIDA 2014 DORICE MOLLEL ATOA MSAADA WA VIFAA TIBA KWA WODI YA WATOTO NJITI

MISS SINGIDA 2014 DORICE MOLLEL ATOA MSAADA WA VIFAA TIBA KWA WODI YA WATOTO NJITI

No comments
By danielmjema.blogspot.com
DSC03176
Miss Singida 2014 Dorice Mollel akizungumza muda mfupi kabla ya kukabidhi vifaa tiba vyenye thamani ya zaidi ya shilingi 1.2 milioni kwenye wodi ya watoto njiti ya hospitali ya mkoa mjini Singida. Miss Singida huyo ambaye mwaka jana alikuwa pia mshindi wa kwanza Miss kanda ya kati na kushika nafasi ya tatu katika shindano la kumsaka Miss Tanzania, amesema ametoa msaada huo kwa sababu na yeye alizaliwa mapacha njiti.
DSC03187
Miss Singida 2014 Dorice Mollel akimkabidhi Kaimu Mganga Mfawidhi Hospital ya Rufaa ya mkoa wa Singida, Dk.Daniel Tarimo, msaada wa vifaa mbali mbali vyenye thamani ya zaidi ya shilingi 1.2 milioni kwa wodi ya watoto njiti.

DSC03191
Kaimu Mganga Mfawidhi Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Singida, Dk.Daniel Tarimo, akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi msaada wa vifaa mbalimbali vya tiba vilivyotolewa msaada na Miss Singida 2014 Dorice Mollel kwenye wodi ya watoto njiti hospitali ya mkoa wa Singida.
DSC03207
Miss Singida 2014 Doris Moleli,akimwangalia mtoto mchanga aliyelazwa kwenye wodi ya uzazi kawaida iliyopo kwenye hospitali ya mkoa mjini Singida.

Miss Tanzania 2013 Happiness Watimanya at the Miss World in London

Miss Tanzania 2013 Happiness Watimanya at the Miss World in London

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com

By Ayoub Mzee –London 

Miss Tanzania 2013 Happiness Watimanya is in town in time for the festive season where she will experience the famous Christmas spirit that can be found in England's capital city. For a little over three weeks, she and the other contestants will experience the wonder of England's vibrant multicultural metropolis as she takes part in the Miss World Challenge Events and prepare herself for the Big Final!
The events start from 20th November, culminating in the Grand Final on 14th December. She is in high spirits and for the first time  Tanzania has a big chance of becoming one of the big three. Tanzanians and friends of Tanzania, there is so much you can do to 


Miss Tanzania 2013 Happiness Watimanya 
Miss Tanzania 2013 Happiness Watimanya at a birthday bash of one of the contestants
Miss Tanzania 2013 Happiness Watimanya on the cat-walk
Happiness Watimanya and colleagues visit a hall of fame
Miss Tanzania 2013 Happiness Watimanya in traditional outfit
Miss Tanzania 2013 Happiness Watimanya and the rest of the 2014 Miss World contestantshelp her out: 
 So how does it work? 
 Simply download the Miss World App, and you will find you have three slots available for your vote. Once you have decided who your top three are, you can lock in your vote and voila!, you have helped your favorite contestants on their way to being the People’s Choice Award Winner! The winner of the People’s Choice Award is announced during the latter stages of the Miss World Final, and the winner, if she is not already selected, will join the final few contestants on stage. These contestants will then face the judges questions before the winner of Miss World 2014 is announced! 

 How many votes do I get? 

 This year, you will be allowed one set of three votes, with a bonus set of three votes if you choose to subscribe to the app, which also includes the full Miss World TV coverage of the competition. The most votes any one contestant can receive from an individual is 2 votes. Each set of votes must be for 3 different contestants. 

 I can’t find the voting page on the App,

 am I doing something wrong? 

 Voting begins on the 20th of November. Until then you will not be able to vote for your favourite contestant. This is to ensure no votes are lost if a contestant has to pull out at the last minute! 

 I haven’t decided yet who my 3rd favourite is, 
when do I have to submit my vote? 

 Don’t worry! You have plenty of time to decide. The app will hold onto your choices until you make your final submission. Voting closes one hour after the start of the Miss World Final Show. Once you have submitted your votes, there is no going back, so make sure you vote right! The time is now to support Tanzania's   beauty at the world stage.

DORIS MOLLEL ACHANGIA VITABU SHULE YA MSINGI MPUNGUZI, DODOMA KWA USHIRIKIANO NA MAK SOLUTIONS LTD

DORIS MOLLEL ACHANGIA VITABU SHULE YA MSINGI MPUNGUZI, DODOMA KWA USHIRIKIANO NA MAK SOLUTIONS LTD

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
1
Doris Mollel akikabidhiwa vitabu 200 na mkurugenzi wa MAK Solutions Bi Meetal Kirubakaran. Vitabu hivyo vilikabidhiwa kwa shule ya msingi Mpunguzi iliyopo Dodoma kama mchango wa kuadhimisha siku ya watoto duniani.(Picha zote na Albert Manifester).
Dodoma, Novemba 2014.
Katika kuadhimisha siku ya watoto duniani inayofanyika tarehe 20 Novemba kila mwaka, Mrembo wa Redds Miss central Zone 2014 Doris Mollel amechangia Vitabu vyenye thamani ya Shilingi Milioni moja (1,000,000/=) katika shule ya msingi Mpunguzi iliyopo katika kijiji cha Mpunguzi mkoani Dodoma.
Doris, ambaye pia ni mshindi wa tatu kwenye Redds Miss Tanzania 2014 amejikita katika sekta ya elimu kama sehemu ya huduma zake za jamii ambapo amedhamiria kuendeleza mchango kwenye elimu ya msingi kwa kuchangia vitabu kwenye shule zenye uhitaji zaidi.
Msaada huo wa Vitabu 200 vya kiada na ziada ameutoa kwa ushirikiano na kampuni ya uuzaji wa Vitabu ya MAK Solutions yenye duka lake Mlimani City jijini Dar es salaam ambapo mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo Bi Meetal Kirubakaran alisema MAK solutions wanafurahi kutoa vitabu hivyo kama mchango wao katika kusaidia sekta ya elimu Tanzania.
2
Doris akijadiliana jambo na Afisa elimu wa mkoa wa Dodoma Bw. Juma Kaponda (Katikati) mjini Dodoma kabla ya kuelekea Mpunguzi. Wa kwanza kushoto ni Afisa elimu - ufundi manispaa ya Dodoma Bw Mnyagatwa Mazengo na anayefuata ni Afisa elimu – Taaluma wa mkoa Bw Eliud Njogela.
Akizungumza kwenye hafla iliyofanyika shuleni hapo, Mollel alisema ‘Ni muhimu kuwajengea watoto wetu utamaduni wa kujisomea tangu wakiwa wadogo ili kuwakuza kukabiliana na changamoto za dunia ya sasa ambayo inahitaji uelewa mpana. Najivunia kuwa sehemu ya kampeni hii na nitaendelea kuongeza jitihada za kuwafikia watoto wengi zaidi’
Afisa elimu wa mkoa wa Dodoma Bw. Juma Kaponda amempongeza Doris kwa juhudi zake za kusadia jamii hasa sekta ya elimu na ameomba wadau wengi kuiga mfano huu kuendeleza sekta hii.
Hafla hiyo ya makabidhiano ilihuduriwa na mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi Mpunguzi Bi Neema Mando, Makamu mwalimu mkuu wa shule Bw Danctan Chipalo, Afisa elimu - ufundi manispaa ya Dodoma Bw Mnyagatwa Mazengo, Afisa elimu – Taaluma wa mkoa Bw Eliud Njogela pamoja na wanafunzi wote wa shule ya Mpunguzi.
3
Alipokuwa njiani kuelekea mpunguzi, Doris alipata nafasi ya kuongea machache na baadhi ya wanafunzi wa vijiji vya jirani.
4
Wanafunzi wakimsikiliza kwa makini.
5
Doris Mollel (kulia) akitia saini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili shuleni Mpunguzi. Kushoto ni Afisa elimu - ufundi manispaa ya Dodoma Bw Mnyagatwa Mazengo na katikati ni mwalimu mkuu wa shule ya mpunguzi Bi Neema Mando.
6
Doris akiuleza uongozi wa shule nia na madhumi ya safari yake. Kushoto ni mwalimu mkuu msaidizi Bw Danctan Chipalo na mwalimu mkuu Bi Neema mando.
7
Afisa elimu - ufundi manispaa ya Dodoma Bw Mnyagatwa Mazengo akimsaidia Doris kuchambua vitabu hivyo kutoka kwenye boksi la MAK Solutions Ltd.
8
Doris akiwaeleza wanafunzi umuhimu wa kupenda kujisomea tangu wakiwa wadogo.
9
Kutoka kushoto: Bw Danctan Chipalo, Bw Mnyagatwa Mazengo Bi Neema Mando na Doris.
10
Doris akiwa na baadhi ya wanafunzi baada ya kugawa vitabu.
11
Wanafunzi wakifurahia vitabu vyao.
12
Akimuelekeza mmoja wa wafunzi juu ya mambo yaliyomo kwenye kitabu cha ‘WATER’
13
Wakiwa na Vitabu.
14
Makabidhiano.
15
Doris akiongea jambo na mwalimu mkuu mara baada ya makabidhiano hayo.
16
Akiwa kwenye picha ya pamoja kwenye viwanja vya shule hiyo muda mfupi kabla ya kuondoka shuleni hapo.

KABAAANG!!! MISS TANZANIA SITTI MTEMVU ALIVUNJA MASHARTI YA.....!

KABAAANG!!! MISS TANZANIA SITTI MTEMVU ALIVUNJA MASHARTI YA.....!

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com

TENA! Saa chache tu baada ya Miss Tanzania 2014 aliyezua tafrani la kuchakachua umri kwa kujipunguzia miaka 2 ya kuzaliwa, Sitti Abbas Mtemvu kujisalimisha kwa kujivua taji mwenyewe, mapya yameibuka na Ijumaa Wikienda lina mzigo mkononi!


Miss Tanzania 2014 aliyevuliwa taji, Sitti Abbas Mtemvu akipanda jukwaani kupata maombi ya Nabii Yaspi Bendera.
YAMEIBUKAJE?
Mapya hayo yameibukia ndani ya Kanisa la Revelation Church lililopo Buza–Kipera jijini Dar kwa Nabii Yaspi Bendera ambaye amezungumzia ishu ya Sitti kujivua  taji mwenyewe.

HUYU HAPA
“Alikuja kwangu nikamwombea, akapata taji. Hata alipopata alikuja kushukuru, nilimwambia aendelee kudumu kwangu hadi atakapokwenda kwenye taji la dunia (Miss World) lakini hakufanya hivyo, akawa haji tena.

“Hivi, nitoe mfano mmoja. Kama mtu akienda kwa mganga kuomba apewe dawa ili apate ujauzito, akishapata akaenda kwa mganga mwingine kuomba amfanyie dawa ili ujauzito huo usitoke. Je, siku ukitoka nani analaumiwa, mganga wa kwanza au wa pili?”
Aliyekuwa Miss Tanzania 2014 akipokea maombi ya nguvu kutoka kwa Nabii Yaspi Bendera

TAFSIRI YAKE HAPA!
Kwa tafsiri rahisi sana ya mazungumzo ya nabii huyo, Sitti alikwenda kanisani kwake akaomba baraka ili ashinde taji la Miss Tanzania, akashinda lakini baadaye alihama kanisa na kwenda kusali kwingine mpaka alipovua taji.

Nabii Yaspi aliandelea kudai kwamba, kama Sitti angeendelea kudumu kwenye kanisa lake na kuombewa maombi ya nguvu, asingevua taji na angefanikiwa kwenda Miss World 2015 ambako pia angetwaa taji la dunia. 
Lakini baada ya kutwaa taji alienda kanisa jingine akiwa na taji lake, matokeo yake mambo yakawa magumu mpaka alipolazimika kuvua taji hilo.

Nabii Yaspi Bendera akimkumbatia Sitti Abbas Mtemvu.

KUMBE ALISHAONYWA 
Habari nyingine kutoka kwa mtu asiye msemaji wa kanisa hilo zinasema kuwa, baada ya kutwaa taji, Sitti alionywa na Nabii Yaspi kwamba kutaibuka vikwazo katika nafasi yake hiyo lakini alichotakiwa kufanya ni kudumu katika maombi ya kanisa hilo ili vikwazo hivyo vifutike lakini kwa sababu hakufanya hivyo matokeo yake ni hayo! 

SITTI AMEFIKAJE HAPA?
Siku chache baada ya Sitti kutwaa Taji la Miss Tanzania 2014 katika shindano lililochukua nafasi ndani ya Ukumbi wa Mlimani City, Dar, Oktoba 11, mwaka huu, yaliibuka madai kwamba, mrembo huyo alichakachua umri akidai ana miaka 23 wakati ana miaka 25.

Mwenyekiti wa kamati ya Miss Tanzania, Hashimu Lundenga akijibu hoja kutoka kwa wanahabari

Sheria za Miss Tanzania, mrembo mwenye miaka 25 haruhusiwi kushiriki mashindano hayo.

Katika madai hayo, ilisemekana kwamba, mrembo huyo alizaliwa Mei 31, 1989 kwenye Hospitali ya Aga Khan jijini Dar. Lakini yeye cheti alichokipeleka kwenye Kamati ya Miss Tanzania akidai alikipata kwa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (Rita) kilionesha mlimbwende huyo alizaliwa Mei 31, 1991 hivyo ana miaka 23.

PASPOTI NDIYO CHANZO
Mazito yote yaliyompata Sitti, chanzo ni hati yake ya kusafiria (paspoti) ambayo ilibandikwa kwenye mitandao ya kijamii ikionesha mrembo huyo ambaye ni binti wa Mbunge wa Jimbo la Temeke kwa tiketi ya CCM, Abbas Mtemvu, alizaliwa Mei 31, 1989.

Mrithi wa Miss Tanzania 2014, Lillian Kamazima akiwa ni mwenye furaha.
KESI BADO MBICHI!
Katika barua yake kwa Kamati ya Miss Tanzania aliyoiandika Novemba 5, mwaka huu na kufika ofisi za kamati hiyo, Novemba 6, mwaka huu, saa 9:25 mchana, Sitti alisema ameamua kwa hiyari yake kuvua taji hilo baada ya kusakamwa na vyombo vya habari kwamba alichakachua umri.

“Leo nalivua taji rasmi nililopewa na binadamu lakini alilonipa mwenyezi Mungu bado ninalo. Mwisho naomba radhi Watanzania wote kwa uamuzi huo niliochukua,” ilisomeka sehemu ya barua hiyo ya Sitti.
Nafasi ya Sitti imetwaliwa na mshindi wa pili, Lilian Kamazima aliyetokea Arusha.

Hata hivyo, kuna ushahidi wa kutosha kutoka Rita na Idara ya Uhamiaji kwamba, umri wa miaka 25 uliopo kwenye paspoti ya kusafiria ya Sitti ambayo imesambaa kwenye mitandao ya kijamii ndiyo sahihi!

Kwa maana hiyo, Sitti kujivua taji anakuwa amemalizana na kesi ya wananchi waliokuwa wakimkomalia, lakini kesi ya kughushi cheti cha kuzaliwa bado inamhusu kwa sababu kwa sheria za Tanzania, mtu akithibitika kudanganya umri kifungo chake ni miaka 3 jela na jamhuri inaweza kumshtaki kwa kusimamia kesi yenyewe.

Miss Lillian Kamazima akipozi.
NI HISTORIA KWA MISS TANZANIA
Hii ni mara ya kwanza katika historia ya mashindano ya Miss Tanzania yaliyoanza nchini mwaka 1994 baada ya kufutwa awali ambapo mshindi wa kwanza anajivua taji ingawa pia haikuwahi kutokea mshiriki kuvuliwa taji kwa kosa lolote lile.

ILIWAHI KUTOKEA MISS KUDANGAYA SHULE
Mwaka 1995, Miss Tanzania alikuwa ni Emily Adolf, mwanafunzi wa kidato cha pili Shule ya Sekondari ya Central, Dodoma. Ushindi wake ulileta malumbano baada ya kubainika alishiriki akiwa mwanafunzi huku akidai alimaliza. Alifukuzwa shule lakini hakuvuliwa taji.

WEMA ALINUSURIKA NA UMRI
Mwaka 2006, Miss Tanzania, Wema Isaac Sepetu naye alinusurika kuvuliwa taji kwa madai kwamba alidanganya umri wake. Wema alidaiwa kushiriki mashindano hayo akiwa na miaka 17, yeye akadai ana 18 lakini vuguvugu la wananchi kumkomalia miaka hiyo haikuwa kama sasa.

SITTI MTEMVU AKUBALI KUACHIA TAJI LA MISS TANZANIA

SITTI MTEMVU AKUBALI KUACHIA TAJI LA MISS TANZANIA

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Mrembo aliyetawazwa umalkia wa Tanzania 2014, 'Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Mtevu (pichani kushoto) leo ametangaza rasmi kujivua taji hilo. Pamoja nae ni Mkurugenzi wa Lino International Agency Hashim Lundenga, ambao ndio waandaaji wa Miss Tanzania akizungumza japo katika moja ya mikutano na waandishi ambayo ilihusiana na taji hilo la Miss Tanzania 2014 kushikiliwa na Sitti ilhali anashutumiwa kudanganya umri.

MISS TANZANIA WATOA MSAADA HOSPITALI YA KILEMA NA MARANGU MOSHI

MISS TANZANIA WATOA MSAADA HOSPITALI YA KILEMA NA MARANGU MOSHI

No comments
By danielmjema.blogspot.com

Washiriki wa Shindano la Redds Miss Tanzania 2014 walitoa misaada ya kijamii katika Hospitali za Misheni Kilema na ile ya K.K.K.T Marangu baada ya kutembelea Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro.


 Mwakilishi wa Kanda ya Ziwa katika Shindano la Redds Miss Tanzania 2014 Dorine Robert akimpa zawadi ya chandarua mgonjwa Jamila Msafiri aliyelazwa katika Hospitali ya Kilema Wilaya ya Moshi Vijijini Mkoani Kilimanjaro jana ambapo warembo 30 wa Miss Tanzania walitoa msaaada mbalimbali ya kijamii hospitalini hapo.
Warembo wakiangalia watoto

WAREMBO MISS TANZANIA WASHUHUDIA UPIMAJI WAGONJWA WA EBOLA UWANJA WA NDEGE WA KIA

WAREMBO MISS TANZANIA WASHUHUDIA UPIMAJI WAGONJWA WA EBOLA UWANJA WA NDEGE WA KIA

No comments
By danielmjema.blogspot.com
 Washiriki wa Shindano la Redd's Miss Tanzania 2014, wakimsikiliza Afisa Mfawidhi, Nisalile Mwangoka aliyekuwa akiwapa maelezo juu ya upimaji wa wageni wanao ingia nchini kupitia viwanja vya ndege unavyofanyika kutumia mashine maalum iitwayo 'Walk Through Thermoscaner', iliyopo uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) wakati warembo 30 wanaowania taji la Miss Tanzania walipotembelea uwanja huo na kujifunza mambo mbalimbali . Warembo hao wapo katika ziara ya kuhamasisha utalii wa ndani kwa kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii nchini.
 Mashine hiyo ikionekana kufungwa juu kuelekea usawa wa kuingilia abiria wanaowasili tka nje ya nchi.
 Namna inavyoonekana baada ya kipimo kuchukuliwa
 Nisalile Mwangoka akionesha kifaa cha zamani cha upimaji ugonjwa wa Ebola ambacho kimeelezwa kuwa licha ya ufanisi lakini kilikuwa kinaweka foleni kwa abiria tofauti na hicho kipya.
 Meneja wa Usalama katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), Kisusi Makomondi akiwapa maelezo washiriki hao wa shindano la Miss Tanzaniua 2014 juu ya shughuli mbalimbali za uwanja huo.

WAREMBO MISS TANZANIA 2014 WAWASILI KAMBINI.

WAREMBO MISS TANZANIA 2014 WAWASILI KAMBINI.

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Na Father Kidevu Blog
Wanyange 30 wanao wanbia taji la Redd's Miss Tanzania 2014 leo wameingia kambini tayari kwa safari ya fainali za Miss Tanzania 2014 zitakazo fanyikia mapema mwezi Oktoba jiji Dar es Salaam.


Warembo hao waliowasdili kwa muda tofauti kuanzaia saa 12 alfajiri ya leo na kupokelewa na waandaaji wa Miss Tanzania katika hoteli ya JB Belmont iliyopo katikati ya jiji la maraha la Dar. 


Warembo kutoka Kanda ya Ziwa walitia fora pale warembo hao walipowasili kambini hapo wakiwa ndani ya gari ya Mshindi wa Kanda ya Ziwa ambayo alizawadiwa hivi kjaribuni katika shindano lao.
 Warembo wakiwasili kambini
 Warembo wa Kanda ya Ziwa wakiteremka katika gari lao baada ya kuwasili na inaelezwa waliendesha kutoka jijini Mwanza.
 Warembo wa KJanmda ya Ziwa wakijiandikisha baada ya kuwasili kambini.
 Warembo wakielekea chumba cha mkutano.
 Warembo wakiwa katika chumba cha semina ambapo maelezo mbalimbali ya ka,mbi yao yalitolewa.
 
  Warembo wakiwa katika chumba cha semina ambapo maelezo mbalimbali ya ka,mbi yao yalitolewa.

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .