Showing posts with label misaada. Show all posts
Showing posts with label misaada. Show all posts

MKURUGENZI WA KAMPUNI YA UJENZI WA BARABARA IRINGA GNSM ATOA MSAADA WA CHAKULA KWA YATIMA TOSAMAGANGA

MKURUGENZI WA KAMPUNI YA UJENZI WA BARABARA IRINGA GNSM ATOA MSAADA WA CHAKULA KWA YATIMA TOSAMAGANGA

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com

MKurungenzi  wa kampuni ya ujenzi  wa barabara Iringa ya GNSM Bw  Geofrey Mungai na mkewe  Sarafina Mungia katikati  wakikabidhi  baada ya misaada  yenye thamani ya zaidi ya Tsh milioni 1 kwa  mlezi  wa  kituo cha yatima Tosamaganga Godfrida Mhongole

Bw Mungai  akishuhudia  jinsi  watoto  wanavyohudumiwa
Bi Sarafina  Mungia na Geofrey Mungai  wakiwatazama wahudumu  wakiwalisha watoto yatima wa Tosamaganga  Iringa
Bw Geofrey Mungai  akisaidia  kuwapa uji  watoto yatima  wa Tosamaganga Iringa baada ya  kumaliza  kuwapa msaada wa chakula  cha Krismas na mwaka mpya

DK. TIZEBA ATOA MISAADA KWA WAHANGA WA MOTO JIMBONI KWAKE

DK. TIZEBA ATOA MISAADA KWA WAHANGA WA MOTO JIMBONI KWAKE

Posted in ,
No comments
By danielmjema.blogspot.com
SAM_0783
Naibu Waziri wa Uchukuzi ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Buchosa, Dk Charles Tizeba akipanda boti kuelekea kisiwa cha Nyamango kulikotokea ajali ya moto kwa ajili ya kukabidhi misaada.

Na Daniel Makaka, Sengerema

NAIBU Waziri wa Uchukuzi ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Buchosa Dk Charles Tizeba ametoa msaada kwa wahanga wa ajali ya moto na nyumba zilizoezuliwa na mvua ya upepo katika kisiwa cha Nyamango kijiji cha Lushamba kata ya Bulyaheke jimbo la Buchosa wilayani Sengerema mkoa wa Mwanza.

Misaada aliyoitoa kwa wahanga hao ni Blanketi mia tatu na Magunia manne ya Unga wa Mahindi na moja la Maharagwe vyote vyenye thamani ya shilingi million tatu na laki tano ambavyo vimetolewa kwa kaya hamsini na moja ambazo zilikumbwa na janga hilo Septemba 19 na 20 mwaka huu.

Akikabidhi misaada hiyo Dk Tizeba aliwataka viongozi kuhakikisha misaada hiyo inawafikia walengwa na siyo vinginevyo lakini pia aliwaasa wahanga hao hao kutumia misaada kwa lengo la kuwasaidia wakati kamati ya maafa wilaya ya Sengerema ikiwa bado inaendelea kufanya tathimini il iione namna ya kuwasaidia.

SAM_0723
Naibu Waziri wa Uchukuzi ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Buchosa, Dk Charles Tizeba akiwa ndani ya boti kuelekea kukabidhi misaada katika kisiwa cha Nyamango jimboni kwake...Serikali itaendelea kusaidia kadri iwezavyo si kwamba watapewa fidia bali ni misaada tu.

Awali Katibu wa kamati ya maafa wilaya Sengerema Bw. Benard Myatilo akitoa taarifa ya wahanga wa tukio hilo alisema kuwa matukio hayo yalitokea kwa nyakati tofauti ambapo Septemba 19 majira ya saa nane usiku kaya 40 ziliteketea kwa moto na chanzo cha moto huo ni kulipuka kwa Kibatari ndani ya nyumba na tukio la pili kaya 11 kuezuliwa na mvua ilyoambatana na upepo likiwemo jengo la kanisa Katoliki kisiwani humo.

Pia alisema kati ya wahanga hao hakuna mtu aliyejeruhiwa katika matukio hayo licha mali zote zilizokuwemo kuteketea ambapo hadi sasa kaya saba hazina mahali pakuishi huku zilizobaki zikihifadhiwa na baadhi ndugu na jamaa wanaoishi katika kisiwa hicho.

SAM_0749
Muonekano wa baadhi ya nyumba zilizoteketea kwa moto katika kisiwa cha Nyamango wilayani Sengerema mkoa wa Mwanza.

SAM_0750
SAM_0753
Kanisa la Roman Katoliki katika kisiwa cha Nyamango lililoezuliwa na upepo ulioambatana na mvua.

SAM_0775
Naibu Waziri wa Uchukuzi ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Buchosa, Dk Charles Tizeba (mwenye suti ya kijivu) akikabidhi misaada ya mablanketi 300 kwa Mwenyekiti wa kijiji cha Lushamba, Deus Bitulo (kulia kwa naibu waziri) huku Mwenyekiti wa CCM tawi la Nyamango, Japhet Kafula akishuhudia tukio hilo
 

TBL YATOA MSAADA WA SH. MIL.24.6 WIKI YA NENDA KWA USALAMA. ZITASAIDIA UPIMAJI AFYA ZA MADEREVA

TBL YATOA MSAADA WA SH. MIL.24.6 WIKI YA NENDA KWA USALAMA. ZITASAIDIA UPIMAJI AFYA ZA MADEREVA

No comments
By danielmjema.blogspot.com
 Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve  Kilindo (kulia), akimkabidhi Mganga Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, SSP Charles Msenga mfano wa hundi yenye thamani ya sh. mil. 24.6 kwa ajili ya Wiki ya Nenda kwa Usalama inayotarajia kuanza hivi karibuni. Anayeshuhudia makabidhiano hayo yaliyofanyika Dar es Salaam jana, ni Kamanda wa Kikosi cha Usalama barabarani, Naibu Kamishna Mohamed Mpinga.
 Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve  Kilindo (kulia), akimkabidhi Mganga Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, SSP Charles Msenga (wa pili kushoto) mfano wa hundi yenye thamani ya sh. mil. 24.6 kwa ajili ya Wiki ya Nenda kwa Usalama inayotarajia kuanza hivi karibuni. Wanaoshuhudia makabidhiano hayo yaliyofanyika Dar es Salaam jana, ni Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Naibu  Kamishna Mohamed Mpinga (wa pili kulia) na Mjumbe wa Kamati ya Usalama Barabarani, Henry Bantu.
 Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve  Kilindo (kushoto) na Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Naibu  Kamishna Mohamed Mpinga wakionesha moja ya fulana zilizotolewa msaada na TBL kwa ajili ya Wiki ya Nenda kwa Usalama katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam jana. TBL ilikabidhi pia hundi yenye thamani ya sh. mil. 24.6 kwa ajili hiyo. 
 Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve  Kilindo (kushoto) na Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Naibu  Kamishna Mohamed Mpinga wakionesha moja ya fulana zilizotolewa msaada na TBL kwa ajili ya Wiki ya Nenda kwa Usalama katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam jana. TBL ilikabidhi pia hundi yenye thamani ya sh. mil. 24.6 kwa ajili hiyo. Fedha hizo pia zitasaidia upimaji wa afya za madereva. (PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG0
 Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve  Kilindo (kulia) akimkabidhi  moja ya fulana na cheti Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Naibu  Kamishna Mohamed Mpinga kwa ajili ya Wiki ya Nenda kwa Usalama katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam jana. TBL ilikabidhi pia hundi yenye thamani ya sh. mil. 24.6 kwa ajili hiyo. Kushoto ni  Mganga Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, SSP Charles Msenga

WAZIRI NYALANDU AMWAGA MSAADA WA MILIONI 10 WA MABATI 420 SHULE ZA SEKONDARI KWA AJILI YA MAABARA

WAZIRI NYALANDU AMWAGA MSAADA WA MILIONI 10 WA MABATI 420 SHULE ZA SEKONDARI KWA AJILI YA MAABARA

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
mwenyekit
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida, Iddy Mnyampanda akizungumza shule ya sekondari Kinyeto.
Na Hillary Shoo, SINGIDA.
Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini Mkoani Singida, Lazaro Nyalandu ametoa mchango wa mabati 420 yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 10 kwa shule mbili za sekondari za Kata za Mtinko na Kinyeto.
Mchango huo ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi zake kwa wananchi wa Jimbo hilo kuchangia katika ujenzi wa maabara mbalimbali kwenye shule za sekondari za Jimbo hilo.
Akikabidhi msaada huo kwa Niaba ya Nyalandu ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Singida Narumba Hanje aliwataka wananchi kuheshimu michango ya Mbunge wao na kuachana na porojo za siasa za mitaani.
kinyeto
Diwani wa Kata ya Kinyeto, Francisco Ng’eni akizungumza kwenye shule ya sekondari Kinyeto wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya mabati 200.
“Nataka niwaulize swali hivi ni wananchi ndio wenye matatizo au ni sisi viongozi, jibu ni rahisi ni sisi viongozi ndio wenye matatizo, haiwezekani Mbunge anatoa msaada mkubwa namna hii halafu watu wanajipitishapitisha wakitukana.” Alisema Hanje kwa hasira.
Aidha alisema wapo watu wanaompaka matope Waziri Nyalandu, lakini matunda yake yanaonekana na anaendelea kutekeleza ahadi zake.
“Mimi inanishangaza sana kuna watu wameanza kujipitisha pitisha huko na wengine wanatukana kisa eti ni kaligi sijuji Mpombo Cup, fanya vitu vionekane sio maneno maneno kaka, na mimi ndiye mtekelezaji mkuu wa Ilani ya Chama Willaya hii.” Alisema Hanje kwa kujiamini.
diwani
Diwani wa Kata ya Kinyeto, Francisco Ng’eni akipokea msaada wa mabati 200 kutoka kwa Mwenyekiti Hanje kwa niaba wa Mbunge wa Jimbo hilo Mhe, Lazaro Nyalandu.
elia
Katibu wa Mbunge Lazaro Nyalandu , Elia Digha, msaidizi wa Mbunge Ellen Mutalemwa wakimsikiliza Mwenyekiti Hanje Kinyeto.
ellen
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye viwanja vya shule ya sekondari ya Mtinko.
hanje
Mwenyekiti wa CCM Singida vijijini, Narumba Hanje akizungumza na wananchi wa Kata ya Mtinko wakati wa kukabidhi mabati 220.
kabidhi
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Singida Vijijini, Narumba Hanje (kulia) akimkabidhi mabati 220 yenye thamani ya shilingi milioni tano Afisa Mtandaji wa Kata ya Mtinko Jimbo la Singida Kaskazini, Eliufoo Mkanga katika hafla fupi iliyofanyika jana katika shule ya Sekondari ya Kata ya Mtinko , mabati hayo yametolewa kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa maabara na Mbunge wa Jimbo hilo Mhe,Lazaro Nyalandu.
maabara
Hili ni jengo la maabara ya sekondari ya Kinyeto likiwa katika hatua ya lenta.
kibao
Kibao kikionesha shule ya sekondari Mtinko.(PICHA ZOTE NA HILLARY SHOO).

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .