DK. TIZEBA ATOA MISAADA KWA WAHANGA WA MOTO JIMBONI KWAKE

Posted in ,
No comments
Wednesday, September 24, 2014 By danielmjema.blogspot.com

SAM_0783
Naibu Waziri wa Uchukuzi ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Buchosa, Dk Charles Tizeba akipanda boti kuelekea kisiwa cha Nyamango kulikotokea ajali ya moto kwa ajili ya kukabidhi misaada.

Na Daniel Makaka, Sengerema

NAIBU Waziri wa Uchukuzi ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Buchosa Dk Charles Tizeba ametoa msaada kwa wahanga wa ajali ya moto na nyumba zilizoezuliwa na mvua ya upepo katika kisiwa cha Nyamango kijiji cha Lushamba kata ya Bulyaheke jimbo la Buchosa wilayani Sengerema mkoa wa Mwanza.

Misaada aliyoitoa kwa wahanga hao ni Blanketi mia tatu na Magunia manne ya Unga wa Mahindi na moja la Maharagwe vyote vyenye thamani ya shilingi million tatu na laki tano ambavyo vimetolewa kwa kaya hamsini na moja ambazo zilikumbwa na janga hilo Septemba 19 na 20 mwaka huu.

Akikabidhi misaada hiyo Dk Tizeba aliwataka viongozi kuhakikisha misaada hiyo inawafikia walengwa na siyo vinginevyo lakini pia aliwaasa wahanga hao hao kutumia misaada kwa lengo la kuwasaidia wakati kamati ya maafa wilaya ya Sengerema ikiwa bado inaendelea kufanya tathimini il iione namna ya kuwasaidia.

SAM_0723
Naibu Waziri wa Uchukuzi ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Buchosa, Dk Charles Tizeba akiwa ndani ya boti kuelekea kukabidhi misaada katika kisiwa cha Nyamango jimboni kwake...Serikali itaendelea kusaidia kadri iwezavyo si kwamba watapewa fidia bali ni misaada tu.

Awali Katibu wa kamati ya maafa wilaya Sengerema Bw. Benard Myatilo akitoa taarifa ya wahanga wa tukio hilo alisema kuwa matukio hayo yalitokea kwa nyakati tofauti ambapo Septemba 19 majira ya saa nane usiku kaya 40 ziliteketea kwa moto na chanzo cha moto huo ni kulipuka kwa Kibatari ndani ya nyumba na tukio la pili kaya 11 kuezuliwa na mvua ilyoambatana na upepo likiwemo jengo la kanisa Katoliki kisiwani humo.

Pia alisema kati ya wahanga hao hakuna mtu aliyejeruhiwa katika matukio hayo licha mali zote zilizokuwemo kuteketea ambapo hadi sasa kaya saba hazina mahali pakuishi huku zilizobaki zikihifadhiwa na baadhi ndugu na jamaa wanaoishi katika kisiwa hicho.

SAM_0749
Muonekano wa baadhi ya nyumba zilizoteketea kwa moto katika kisiwa cha Nyamango wilayani Sengerema mkoa wa Mwanza.

SAM_0750
SAM_0753
Kanisa la Roman Katoliki katika kisiwa cha Nyamango lililoezuliwa na upepo ulioambatana na mvua.

SAM_0775
Naibu Waziri wa Uchukuzi ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Buchosa, Dk Charles Tizeba (mwenye suti ya kijivu) akikabidhi misaada ya mablanketi 300 kwa Mwenyekiti wa kijiji cha Lushamba, Deus Bitulo (kulia kwa naibu waziri) huku Mwenyekiti wa CCM tawi la Nyamango, Japhet Kafula akishuhudia tukio hilo
 

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .